Amani ya Akili kwa Mmiliki

Uko kazini, nyumbani, kanisani, likizoni — biashara yako inaendelea.

Hata ukiwa mgonjwa au safarini, fuatilia fedha, stock, oda na wafanyakazi wako kutoka popote ulipo. Ripoti inakufikia WhatsApp kila siku — bila wewe kuwepo dukani.

RIPOTI YA LEO
Jumatatu · 19/07/2026

MauzoTZS 184,000
Matumizi (posho, nauli)TZS 96,500
Stock iliyobakiChini ya kiwango

SalioTZS 87,500
⚠ Stock ya sukari imefikia kiwango cha kuagiza upya
"

Biashara ambayo haiwezi kujiendesha bila wewe, si biashara bali ni ajira uliyojiajiri mwenyewe.

Sehemu Zote, Biashara Moja

Kila kitu unachosimamia kwa mkono, sasa kwenye simu.

Inafaa biashara ndogo za aina yoyote — duka, hoteli, lodge, minisupermarket, famasi, genge na nyinginezo — kila moja ikishughulikia kazi ya kila siku ya biashara yako.

Duka Hoteli Lodge Minisupermarket Famasi Genge na nyingine
Fedha

Hesabu ya fedha na faida

Weka float ya asubuhi, ingiza mauzo na matumizi. Ukitumia zaidi ya unavyopata, unaonywa papo hapo.

Wafanyakazi

Ufunguzi na ufungaji wa duka

Orodha ya kazi za kufungua na kufunga — mahudhurio, usafi wa sakafu na rafu, muda wa kufungua.

Oda

Oda na mahitaji ya ununuzi

Mmiliki anaona oda zilizolala, oda mpya zilizoingia, na mahitaji ya kununua ya siku hiyo — yote sehemu moja.

Masoko

Utangazaji wa kila siku

Inawakumbusha na kufuatilia kama wafanyakazi wamepost WhatsApp Status ("Tupo Wazi") na Instagram kila siku.

Wateja

Ufuatiliaji wa wateja

Inawahimiza wafanyakazi kutembelea wateja wapya, kupiga simu wateja wa siku zote kujua status ya oda yao, na kuomba oda mpya.

Stock

Ufuatiliaji wa stock

Weka kiwango cha chini kwa kila bidhaa (pcs, kg, lita) — unaonywa kabla haijaisha kabisa.

Ripoti

Ripoti moja ya jumla

Muhtasari wa siku nzima — fedha, stock, wafanyakazi — kwa picha za ushahidi, tayari kutumwa.

Nje ya Mtandao

Inafanya kazi bila intaneti

Faili moja, kwenye simu yako. Data haiendi kwa mtu mwingine mpaka wewe mwenyewe utume.

Jinsi Inavyofanya Kazi

Dakika tano za kuanza, kila siku baada ya hapo ni haraka.

Haihitaji intaneti ya kudumu

Inafanya kazi kwenye simu bila mtandao. WhatsApp inahitajika tu wakati wa kutuma ripoti.

Data inabaki kwenye simu

Hakuna seva ya nje inayohifadhi taarifa za duka lako bila ridhaa yako.

Inafanya kazi kwa Kiswahili

Imejengwa kwa lugha na mazingira ya wafanyabiashara wa Tanzania.

Anza kusimamia biashara yako leo.

Chagua mpango unaokufaa — lipa kila mwezi, au lipa miezi 6 mara moja upate bei nafuu.

Kila Mwezi
TZS 30,000/mwezi

Lipa mwezi mmoja mmoja, jisitishe wakati wowote.

Pata Zana — Lipa Sasa
M-Pesa Lipa Namba
51088025
Airtel Money
0699 354 779